Home Yanga SC SABABU YA DITRAM NCHIMBI KUTOFUNGA HII HAPA

SABABU YA DITRAM NCHIMBI KUTOFUNGA HII HAPA


 MSHAMBULIAJI wa Yanga, Ditram Nchimbi amesema kuwa sababu ya kushindwa kufunga ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ni presha pamoja na ukubwa wa timu hiyo.

Msimu huu wa 2020/21 ndani ya Yanga nyota huyo hajafunga bao huku timu yake ikiwa imefunga jumla ya mabao 34 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Yeye amehusika kwenye mabao mawili ambapo alitengeneza pasi za mabao kwa Michael Sarpong wakati wakishinda bao 1-0 dhidi ya Biashara United na Mukoko Tonombe wakati Yanga ikilazimisha sare ya kufungana mabao 3-3.

Msimu huu amecheza mechi 16 na msimu uliopita alipoibuka ndani ya Yanga akitokea Polisi Tanzania alicheza jumla ya mechi 11 na alimaliza akiwa na mabao sita, mawili ilikuwa ni ndani ya Yanga na manne alifunga alipokuwa Polisi Tanzania.

Nchimbi amesema:”Presha ndani ya timu pamoja na ushindani ni sababu inayonifanya nishindwe kufunga ila pia sikumbuki mara ya mwisho kufunga ilikuwa lini,”.

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara imecheza mechi 21 na imekusanya pointi 49.

SOMA NA HII  KISA SIMBA...BANGALA AENDA KWAO CONGO 'KUJIBUSTI'..NADI AKUNA KICHWA..AFUNGUKA HAYA...