Home Simba SC SIMBA QUEENS HAKUNA KULALA, WAPIGA TIZI MARA TATU KWA WIKI

SIMBA QUEENS HAKUNA KULALA, WAPIGA TIZI MARA TATU KWA WIKI

 


KAMA ulidhani Simba Queens watabweteka na likizo ya kusimama kwa Ligi Kuu ya Wanawake, basi utakuwa umekosea sana kwani kikosi hicho kimemua kufanya mazoezi mara tatu kwa wiki kabla ya kuanza tena rasmi kambi ya ujumla.

Mpaka Ligi Kuu soka ya Wanawake inakwenda mapumziko baada ya michezo 11 kupigwa, tayari mabingwa hao watetezi walikuwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zao 29.

Akizungumzia mipango waliyonayo kocha mkuu wa kikosi cha Simba Queens, Mussa Mgosi amesema wamefikia maamuzi hayo ili kuhakikisha kikosi chao kinasalia katika hali ya ushindani ili kufanikisha mpango wao wa kutetea ubingwa wao.

“Baada ya ligi kusimama kwa muda kufuatia kukamilika kwa mzunguko wa kwanza, kikosi chetu kiliazimia kusalia katika hali ya ushindani ambapo tunaendelea na mazoezi tukifanya mara tatu kwa siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa,”

SOMA NA HII  AHMED ALLY AWEKA WAZI ISHU YA KIMATIFA