Home Simba SC SIMBA YATINGA MAKAO MAKUU,DODOMA,KUIBUKIA BUNGENI

SIMBA YATINGA MAKAO MAKUU,DODOMA,KUIBUKIA BUNGENI

KIKOSI cha Simba kinachonole na Kocha Mkuu, Didier Gomes na msaidizi wake Seleman Matola leo kimewasili salama makao makuu ya nchi Dodoma.

Jana wachezaji walilipoti kambini baada ya kupewa mapumziko ya siku moja baada ya kukamilisha kusepa na taji la Simba Super Cup Januari 31, Uwanja wa Mkapa.

Leo watakwenda pia Bungeni kwa ajili ya kupewa baraka na Wabunge kuelekea Kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Februari 12 kitacheza na AS Vita ya Congo.

Kesho Uwanja wa Jamhuri Dodoma kitakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji.

SOMA NA HII  GOMES: WACHEZAJI WALIKOSA NAFASI NYINGI ZA WAZI MBALI NA PENALTI