Home Simba SC GOMES: WACHEZAJI WALIKOSA NAFASI NYINGI ZA WAZI MBALI NA PENALTI

GOMES: WACHEZAJI WALIKOSA NAFASI NYINGI ZA WAZI MBALI NA PENALTI


 DIDIER Gomes,  Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mbali na wachezaji wake kukosa penalti kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons bado walikosa nafasi nyingi za wazi jambo ambalo watalifanyia kazi.


Wakati ubao ukisoma Simba 1-1 Tanzania Prisons,  Chris Mugalu alipiga penalti iliyoishia kwenye mikono ya kipa namba moja wa Prisons,  Jeremiah Kisubi.


Jitihada za Simba kutafuta bao zlikuja kuonekana dakika ya 90+5 kupitia kwa Luis Miquissone na kufanya Simba ipate pointi moja kwa kuwa ilifungwa dakika ya 56 na Salum Kimenya kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya 18.


Raia huyo wa Ufaransa amesema kuwa wamekuwa wakifanyia mazoezi mipira iliyokufa mara kwa mara ila imekuwa ngumu kwao kupata ushindi jambo ambalo atalifanyia kazi wakati ujao.


“Ukiachana na kukosa penalti bado wachezaj walitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia hivyo ni kazi kwetu kuyafanyia kazi makosa kwa ajili ya wakati ujao.


“Kukosa ama kupata kwetu ni darasa kwa ajili ya muda mwingine.  Nina amini kwamba kuna kitu ambacho wachezaji wamekipata na wanastahili pongezi kwa kuwa walipambana, “.


Simba inafikisha pointi 46 ikiwa nafasi ya pili huku vinara ni Yanga wana pointi zao 50 kibindoni.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AANZA KUTOA LUGHA TATA,,,,, ISHU IKO HIVI