Home Simba SC YANGA WAFUNGUKIA ISHU YA USAJILI WA LUIS ANAYECHEZA SIMBA

YANGA WAFUNGUKIA ISHU YA USAJILI WA LUIS ANAYECHEZA SIMBA

 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa haukuwa na mpango wa kumsajili kiungo mwenye kasi ndani ya uwanja, mjanjamjanja ndani ya uwanja Luis Miquissone.

Awali ilielezwa kuwa Yanga walikuwa kwenye hesabu za kuisaka saini ya nyota huyo ila walizidiwa ujanja na watani zao wa jadi zama zile alipokuwa anacheza ndani ya timu ya UD Songo.

Kwa sasa yupo Simba ambayo inapambania kutetea taji la Ligi Kuu Bara na kesho Februari 4 itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Dodoma Jiji, mchezo wa ligi.

Mjumbe wa Kamati ya Usajili ndani ya timu ya Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa timu hiyo inayoongoza ligi kwa sasa amesema kuwa hawakuwa na mpango na Luis.

“Simba walikuwa wa kwanza kumfuata Luis ila sisi hatukuwa na mpango wa kusmajili mchezaji huyo jambo ambalo limefanya awe pale ambapo alikuwa anahitajika.

“Ni tetesi ambazo zilikuwa zinaeleza na kulipa nguvu suala hilo hivyo hakuna jambo ambalo lilikuwa linaendelea juu yetu,” amesema.

Luis kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara ni namba mbili wa kutengeneza pasi za mwisho akiwa nazo saba na ametupia bao moja.

Namba moja ni Clatous Chama ambaye ametoa pasi nane na amefunga mabao sita kibindoni.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA KIWANGO CHA SAKHO SIKU ZA HIVI KARIBUNI...PABLO AKUNA KICHWA WEE...KISHA ANENA HAYA..