Home Uncategorized YANGA YAZIDIWA UJANJA KWA SIMBA YAPISHANA NA KIUNGO HUYU FUNDI WALIYEKUWA WAKIMPIGIA...

YANGA YAZIDIWA UJANJA KWA SIMBA YAPISHANA NA KIUNGO HUYU FUNDI WALIYEKUWA WAKIMPIGIA HESABU


IMEELEZWA kuwa Said Ndemla ameongezewa mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kukipiga kwenye klabu hiyo kwenye msimu ujao baada ya kufikia muafaka mzuri na mabosi wake.

Awali, kiungo huyo alikuwa anatajwa kutimkia Yanga ambayo ilikuwa inatajwa kuwania saini yake kwa ajili ya kuiimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kiungo huyo amebakishwa kutokana na nidhamu kubwa aliyoionyesha akiwa na timu hiyo licha ya kutokuwepo katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kinachonolewa na Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.
Aliongeza kuwa kingine kilichombakisha ni uwepo wa viungo wakabaji wachache katika timu hiyo, licha ya kuwepo mipango ya kushusha kiungo mwingine mkabaji wa kimataifa mwenye uwezo mkubwa zaidi yake.
“Viongozi wamekubaliana kuwabakisha wachezaji wao waliowalea tangu wakiwa wadogo U20 kwa lengo la kutoondoka ndani ya kikosi hicho kutokana na uvumilivu waliokuwa nao wa kutoihama timu hiyo ambao ni Ndemla na Mkude (Jonas).
“Hivyo viongozi wamekubaliana kumbakisha, lakini amebakishwa kwa makubaliano ya kupambana katika timu ili apate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
“Ndemla amekubaliana na hayo yote waliyokubaliana nayo huku akiomba mkataba wake uwe wa wazi utakaomruhusu kuondoka muda wowote kama akipata timu nje ya nchi,” alisema mtoa taarifa huyo.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa hivi karibuni aliwahi kuliambia Championi kuwa: “Kama uongozi tumepanga kuwabakisha wachezaji wote ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu kwa gharama yoyote lengo ni kuhakikisha tunasuka kikosi imara kitakachofanya vizuri katika msimu ujao.”
SOMA NA HII  YANGA NA MCHONGO HUU LIGI YA MABINGWA