Home Habari za michezo BAADA YA ROBO FAINAL KUPANGWA….CAF WAIRUDUSHIA SIMBA HESHIMA YA MWAKA 2003….MPANGO UKO...

BAADA YA ROBO FAINAL KUPANGWA….CAF WAIRUDUSHIA SIMBA HESHIMA YA MWAKA 2003….MPANGO UKO HIVI…

Habari za Simba

Klabu ya Simba imerudishwa tena nchini Morocco ambapo katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika imepangwa kucheza na mabingwa watetezi wa kombe hilo, Wydad Casablanca.

Simba ambaye ametoka kucheza kundi moja na Raja Casablanca ya huko huko Morocco, sasa ataanzia nyumbani katika Dimba la Mkapa na kumalizia nchini Morocco.

Simba SC vs Wydad Casablanca
Al Ahly vs Raja Casablanca
CR Belouizdad vs Mamelodi Sundowns
JS Kabyle vs ES Tunis

Droo ya nusu fainali:

Mshindi kati ya Kabyle na ES Tunis atakutana na mshindi kati ya Al Ahly na Raja Casablanca wakati mshindi kati ya Simba ma Wydad atakutana na mshindi kati ya Belouizdad na Mamelodi Sundowns.

Michezo ya robo fainali itapigwa tarehe 21 na 22 Aprili 2023 na marudiano ni tarehe 28 na 29 Aprili, 2023.

Kitendo cha Simba kukutana na Wydad ambao ni mabingwa watetezi , kinafafa na tukio kama hili miaka 20 iliyopita ambapo wlaikutana na Zamaleki mwaka 2003 ambapo walikuwa mabingwa.

Katika mchezo huo kama ulivyo mchezo ujao, Simba walianzia nyumbani na kupata ushindi wa goli 1-0 , kabla ya kwenda kufungwa goli 1-0 nchini Misri matokeo ambayo yalipelekea timu hizo kwenda kwenye hatua ya matuta.

Kilichofanyika kwenye matuta, mpaka sasa ni mkosi mtupu kwa Zamaleki kwani toka wakati huo haijawahi kurudi tena kwenye ubora wake na kushinda taji hilo.

SOMA NA HII  ZINGATIA ALAMA HIZI ZA USHINDI KWENYE JACKPOT LAB NDANI YA MERIDIANBET...