Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA JWANENG….AHMED ALLY AMTAJA ATAKAYEWAHUJUMU SIMBA…

KUELEKEA MECHI NA JWANENG….AHMED ALLY AMTAJA ATAKAYEWAHUJUMU SIMBA…

Habari za Simba leo

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ametoa hatadhari kwa yoyote ambaye atatia mkono kutaka kuihujumu na kuiangusha timu hiyo ili asiende hatua ya robo fainali.

Ameshusha presha mashabiki kuwaambia Simba kama watakuwa kitu kimoja na kushikamana hakuna yoyote ambaye atatia mkono katika mchezo wao , na atakayekuwa ameingilia mechi hiyo watakuwa wamemkaribidha wenyewe.

Kauli hiyo ameitoa Ahmed katika uzinduzi wa kuelekea mchezo mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, alisema yoyote atakayegusa mechi zao basi hatakuja kusahau na kizazo chake.

Amesema wanakusanya nguvu zao na kuwa kitu kimoja na kusimama imara na hakuna mtua ambaye atatia mkono mechi zao ikiwemo ya Jumamosi, dhidi ya Jwaneng Galaxy.

“Mpira ni burudani lakini ni vita , unapoingia katika matokeo basi tunaingia katika vita na hatutacheza na mtu, yoyote anayejifanya kiherehere kucheza mechi yetu tutaruka naye vibaya .

Hii wiki tupo kwenye vita kila mmoja awe mkali, tupigane vita vya ardhini, majini, angani kila Mwanasimba abebe siraha ya kupigania Simba inaingia robo fainali.

Mashabiki wa Simba unatakiwa kupambana kwenye vita hii na siraha yake ni kujitokeza siku ya jumamosi kujitokeza uwanjani kwa wingi kuipeleka Simba robo fainali ,” amesema Ahmed.

Amewatoa hofi wanasimba ambao wameingia na ubaridi juu ya mechi ya Jumamosi, maandalizi yamefanyika na yanaendelea kufanyika kwa kile kinachowezekana kutafuta ushindi dhidi ya Jwaneng Galaxy.

“Kwenda robo fainali kunategemea wanasimba wenyewe wangeunganisha nguvu ya pamoja na kwenda Benjamin Mkapa kwa pamoja basi Jwaneng Galaxy atakutana na kifo kibaya sana kama kile alichokutana nacho Horoya FC msimu uliopita.

Jumamosi katika uwanja wa Mkapa tunaenda katika maisha yetu kufanya yale ambayo tumezoea kufNya kuingia katik robo fainali ya tano ya michuano ya kimataifa (CAF),” alisema Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano.

Alieleza kuwa timu ya Abdelhak Benchikha inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo, wakumbuke Simba imezoea kuingia robo fainali na wanaenda kwa mara ya tano katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Simba inapotaka robo fainali basi hakuna timu ambayo itakayowazuia, Jwaneng Galaxy wamekuja katika wakati mbaya, kwa sababu inahitaji kuendelea katika maisha yao na kulipa kisasi.

Iwe iwavyo jua mvua lazima Jwaneng Galaxy wake kifo kibaya kuhakikisha Simba inaenda kucheza hatua ya robo fainali ya nne katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hatuwezi kupoteza mara mbili kwa timu mmoja, hakuna timu yoyote ambayo inaweza kumfunga Simba mfululizo, kama wametufunga 2021 sasa imefika zamu ya Jwaneng Galaxy,” amesema Ahmed.

Ameeleza kuwa licha ya kucheza na Jwaneng Gallaxy lakini wamepata ugenini kutoka nchini Morocco, ambaye mwakilishi wa Wydad Casablanca wapo nchini kufatilia mechi yao Simba na Jwaneng Gallaxy kama kuna viashiria vya upangaji matokeo.

“Tumewakaribisha na sio mtu mmoja pekee wakitaka kuja wote tuna wakaribisha kwa sababu Wydad Casablanca walipotea wenyewe na kupoteza mabao 2 hapa nyumbani, hivyo hata Jwaneng Galaxy watakutaka na balaa sisi tunahitaji bao 1-0 tu itupelele robo fainali,” amesema Meneja huyo.

SOMA NA HII  UKWELI MCHUNGU...ILE YA MORRISON SAWA...LAKINI YA SAKHO MHHHH.....'VAR ILIFUNIKWA KITAMBAA'...

2 COMMENTS