Home Habari za michezo UKWELI MCHUNGU…ILE YA MORRISON SAWA…LAKINI YA SAKHO MHHHH…..’VAR ILIFUNIKWA KITAMBAA’…

UKWELI MCHUNGU…ILE YA MORRISON SAWA…LAKINI YA SAKHO MHHHH…..’VAR ILIFUNIKWA KITAMBAA’…


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Simba wameanza vyema kwa ushindi wa bao 1-0 katika hatua ya robo fainali dhidi ya timu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Mchezo huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, juzi, Jumapili usiku ambapo bao la Simba lilifungwa na beki wa kulia, Shomari Kapombe kwa njia ya penalti.

Pamoja na bao hilo kuamsha furaha kwa mashabiki wa Simba, kocha msaidizi wa  Orlando Pirates, Mandla Ncikazi alilalamikia penalti iliyotolewa na mwamuzi wa kati, Haythem Guirat kutoka Tunisia kuwa aliipendelea Simba kwa kuizawadia tuta.

Mbali na mwamuzi huyo wa kati, waamuzi wengine walikuwa Khalil Hassani ambaye pia anatoka Tunisia na Samuel Pwadutakam wa Nigeria. Mwamuzi wa akiba au ‘fourth official’ alikuwa Ahmed Elghandour kutoka Misri.

Waamuzi wa teknolojia ya usaidizi wa uamuzi (VAR) walikuwa Ahmed Elghandour ambaye alisaidiwa na Youssek Elbosaty. Waamuzi hao wote wanatoka Misri.

Kocha huyo alisema pia mwamuzi hakutenda haki kwani hakujiridhisha kwa kutumia VAR iwapo kweli ilikuwa ni penalti halali.

Ncikazi alisema hakukuwa na sababu zozote zilizomfanya mwamuzi huyo kutotumia VAR katika mechi hiyo na kusema kwa ujumla pamoja na kufungwa VAR haikutumika kabisa.

Kocha huyo alisema kuwa penalti ya Bernard Morrison haikuwa sahihi kwani mchezaji wao alikuwa wa kwanza kuucheza mpira na ilipaswa kuwa kona.

Malalamiko mengine ya kocha huyo ni kitendo cha mwamuzi huyo kuwanyima penalti ya wazi ambayo walistahili kuipata katika mchezo huo.

Kwa ufupi, mchezo huo ulikuwa na matukio kadhaa ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya mpira wa miguu Tanzania, mashabiki wangeshuhudia ukitolewa uamuzi kwa njia ya VAR.

Moja ya tukio hilo lilimhusisha kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Ousmane Sakho ambaye aliangushwa ndani ya eneo la hatari (penalti) na mchezaji wa Orlando Pirates kipindi cha kwanza.

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGWA NA YANGA LEO....KIBARUA CHA PABLO KIPO REHANI SIMBA....MUDA WOWOTE 'KITANUKA' HUKOO...