Simba SC

KAGERE BADO ANAWAZA KIATU CHAKE

admin March 2, 2021 11:47 am

 

MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba, amesema bado anaamini ataendelea kufunga mabao kila atakapopata nafasi ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mfungaji bora msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara.

Ikiwa ataweza kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo msimu huu wa 2020/21, Kagere atakuwa ameweka rekodi ya kutwaa tuzo hiyo mara tatu mfululizo kwa kuwa tayari amefanya hivyo msimu wake wa kwanza 2018/19 akitupia mabao 23 na msimu wa 2019/20 alitupia mabao 22.

 Ushindani kwenye kucheka na nyavu msimu huu umekuwa mkubwa ambapo Kagere akiwa na mabao tisa kabla ya mechi ya jana, anayemfuatia ni John Bocco wa Simba mwenye mabao nane, huku Price Dube wa Azam FC, Adam Adam wa JKT Tanzania na Meshack Abraham wa Gwambina, kila mmoja akitupia mabao saba.

 “Ni msimu wa kipekee ndani ya ligi na kila mchezaji anafanya vizuri, hilo lipo wazi.“Kwangu ninapambana ili kufunga pale ambapo nitakuwa ninapata nafasi. Malengo ni kuwa mfungaji bora,” alisema Kagere.

ORODHA YA MASTAA TISA NDANI YA SIMBA AMBAO MIKATABA YAO ITAFIKA UKINGONI MSHAMBULIAJI WA YANGA ATOA AHADI YA MABAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply