Yanga SC

Hatma Ya Pacome Mashakani, Yanga Kuboresha Huduma

Vardo July 1, 2026 3:27 pm

BAADA ya kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Pacôme Zouzoua, kuvunjika eneo ya enka, uongozi wa klabu hiyo umeanza harakati za kuhakikisha mchezaji huyo anapatiwa matibabu ya haraka na ya kitaalamu ili kumrejesha uwanjani kwa usalama.

Pacôme amevunjika katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam, baada ya kuchezewa rafu kali akiwa kwenye harakati za kuwania mpira

Tukio hilo lilitokea jana katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali kuanzia dakika za mwanzo hadi mwisho, ambapo mchezaji huyo alilazimika kutolewa uwanjani baada ya kushindwa kuendelea kutokana na maumivu makali ya enka.

Inadaiwa kuwa jeraha hilo lilitokana na rafu iliyofanywa na mchezaji wa JKT Tanzania, Hassan Wahabi, wakati wakiwania mpira, hali iliyoacha taharuki kwa wachezaji na benchi la ufundi la Yanga pamoja na mashabiki waliokuwa uwanjani.

Akizungumzia hali ya mchezaji huyo, Msemaji wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Ali Kamwe, amesema Pacôme ameumia vibaya na kwa sasa klabu inasubiri taarifa rasmi za kitabibu kubaini ukubwa halisi wa jeraha hilo

Kamwe amesema tukio hilo lilikuwa la hatari na limeacha wasiwasi mkubwa ndani ya benchi la ufundi, hasa kutokana na umuhimu wa mchezaji huyo katika kikosi cha Yanga.

Ameongeza kuwa kipaumbele cha klabu kwa sasa ni kuhakikisha Pacôme anapata matibabu sahihi na ya haraka, huku Yanga ikiendelea kuandaa mipango ya huduma za kitabibu kulingana na ushauri wa madaktari bingwa.

Kiungo Yanga Afunguka Ukweli Msimu Mpya Na Hatma Yake Pacome Afanyiwa Upasuaji, Wiki Sita Chini Ya Uangalizi