Michezo

Kawhi Leonard Arejea Raptors Baada Ya Clippers Kumuuza

Vardo July 1, 2026 3:45 pm

VORZEL, UKRAINE: BINGWA wa uzito wa juu duniani, Oleksandr Usyk anataka kuyaachia mataji yake ili kutoa nafasi kwa mabondia wengine wayashindanie, huku mshkaji wake wa mazoezini, Anthony Joshua, akilenga kutimiza ndoto mpya ya kutwaa ubingwa wa dunia.

Bondia huyo ndiye bingwa anayeshikilia mataji ya ngumi za uzito wa juu duniani yanayotambuliwa na WBA, WBC pamoja IBF.

Usyk aliamua kutokubali pambano dhidi ya mpinzani wake wa lazima aliyepangiwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBC), Agit Kabayel, na hivyo ameamua kuachia mataji yake yote ya dunia ya uzito wa juu.

Bingwa huyo wa dunia wa mataji yaliyounganishwa alikuwa ameonyesha utayari wa kupambana na bondia huyo wa Ujerumani ambaye hajawahi kupoteza pambano, lakini baada ya kutoka sare na Rico Verhoeven, amebadilisha mipango yake.

Na sasa Usyk anajiandaa kupigana pambano moja la mwisho katika uzito wa juu ambalo linaweza kuwa dhidi ya Deontay Wilder, mpinzani ambaye yupo tayari kukutana naye nchini Marekani. Uamuzi wake wa kuachia mataji ulizua mshangao mkubwa katika ulimwengu wa ngumi, hasa kutokana na mapambano makubwa yaliyokuwa yanatarajiwa.

Hata hivyo, akiwa na umri wa miaka 39, meneja wake Sergey Lapin amesema Usyk anastahili kuwa na uhuru wa kuamua mustakabali wa kazi yake bila kulazimishwa na masharti ya kutetea mataji.

Lapin alisema: “Alifanya uamuzi wa makusudi wa kuachia mataji yake ya ubingwa ili kuleta uhai mpya katika uzani wa juu. Hatua hiyo inawapa mabingwa wapya nafasi ya kujidhihirisha na kusaidia kuendeleza mchezo wa ngumi.

“Sasa anataka yeye mwenyewe aamue jinsi sura ya mwisho ya maisha yake ya ngumi itakavyokuwa, badala ya kuachiwa mazingira au masharti ya kutetea mataji kuamua kwa niaba yake.”

Kutakuwa na kipindi cha kuvutia katika uzani wa juu, huku Agit Kabayel akiwa mnufaika wa kwanza wa uamuzi wa Usyk baada ya kutangazwa kuwa bingwa wa WBC. Kwa sasa, Kabayel anamiliki taji la WBC sambamba na Daniel Dubois, ambaye alitwaa ubingwa wa WBO mwezi Mei.

Mabondia Moses Itauma, Frank Sanchez na Murat Gassiev pia wanatarajiwa kujipanga ili kupata nafasi ya kuwania mataji hayo katika wiki zijazo.
USYK ATAKA JOSHUA AWE BINGWA

Sababu nyingine inayodaiwa kumfanya Usyk ayaachie mataji yake ni kumsaidia rafiki yake na mpinzani wake wa zamani, Joshua, kupata nafasi ya kurejea kileleni na kuwa bingwa wa dunia.

Wawili hao wamekuwa wakifanya mazoezi pamoja katika miezi ya hivi karibuni, huku Joshua akitarajiwa kurejea ulingoni mwezi Julai.

Licha ya kusaini mkataba wa kupambana na Tyson Fury, Joshua amesema lengo lake kubwa ni kuwa bingwa wa dunia kwa mara ya tatu.

Usyk anaamini kabisa kuwa Joshua ana uwezo wa kurejea kileleni mwa mchezo huo. Alisema: “Sidhani kama Anthony atakuwa bingwa wa dunia wa mataji yote. Najua Anthony atakuwa bingwa wa dunia wa mataji yote.

“Siyo mpinzani wangu tena. Si adui yangu. Yeye ni mshirika wangu, ni ndugu yangu.

“Kwa sababu najua yeye ni mashine. Sasa anapaswa kufanya kazi kwa bidii. Lazima abadili baadhi ya mambo. Lakini ninaamini hilo linawezekana.”

Mbappe Anavyomtishia Messi Kiatu Cha Dhahabu Kila Mechi ni Fainali, Presha Yaongezeka Taji la Dunia