KOCHA Mkuu wa Ihefu FC, Zuber Katwila amesema kuwa anatambua ushindani ni mkubwa ndani ya uwanja ila watapambana kufanya vizuri.
Kwa sasa Ihefu inapambana kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa baada ya kupanda ndani ya ligi nafasi yake kupanda ndani ya 10 bora imekuwa ngumu.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 imekusanya pointi 20 ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo.
Ni timu nne msimu huu zitashuka jumlajumla kwa zile ambazo zitashika nafasi ya 15 maka 18 huku zile za nafasi ya 16 na 17 zitacheza play off na timu mbili zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa tayari wachezaji wameanza kuelewa kile ambacho wanafundishwa jambo linalowapa imani ya kubaki ndani ya ligi.
“Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji kufanya vizuri hilo lipo wazi hata sisi pia tunapambana kupata matokeo chanya kwani hatuna mpango wa kushuka.
“Mashabiki waendelee kutupa sapoti bado kuna mechi za kucheza ambapo tunaamini kupitia hizo tutapata matokeo ambayo yatatutoa hapa tulipo,”.