Uncategorized

MBAPPE AMKOMALIA NEYMAR AMTAKA ABAKI PSG

admin August 3, 2019 8:12 am


MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Paris Saint Germain (PSG), Kylian Mbappe amesema kuwa anataka kumuona mchezaji mwenzake Neymar Jr anabaki ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Brazil ambaye alijiunga na PSG akitokea Barca kwa dau lililoweka rekodi ya pauni milioni 222 mwaka 2007 hakuwa sehemu ya maandalizi ya kikosi Kwa ajili ya msimu ujao akiamini anarejea Barcelona.

Mpaka sasa PSG wanasema hakuna dili yoyote waliyoipata juu yake na Mbappe amesema anataka kumuona ndani ya kikosi. 

“Kila mmoja anajua juu ya hali yake Kwa sasa, sihataji kuona akiondoka ndani ya kikosi chetu Kwa sasa, anajua namna ninavyofikiria juu yake pamoja na hali yake,” amesema. 

Neymar amekuwa akihusishwa kurejea ndani ya kikosi chake cha zamani cha Barcelona jambo ambalo bado halijawekwa wazi na viongozi.

MESSI ASIMAMISHWA KUSHIRIKI MICHUANO YA KIMATAIFA MIEZI MITATU KUMUONA SIBOMANA, JUMA BALINYA NI BUKU TANO TU TAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply