Home Ligi Kuu DABI YA YANGA PRINCESS V SIMBA QUEENS KUANZA KUCHORA RAMANI YA BINGWA

DABI YA YANGA PRINCESS V SIMBA QUEENS KUANZA KUCHORA RAMANI YA BINGWA

 

EDNA Lema, Kocha Mkuu wa Yanga Princess,  amesema kuwa anaamini mchezo wao dhidi ya Simba Queens,  Machi 5 utakuwa na ushindani mkubwa ila wao wanahitaji pointi tatu. 


Itakuwa ni dabi ambayo itaanza kuchora ramani ya bingwa ajaye kwa kuwa ushindani msimu huu wa 2020/21 umekuwa ni mkubwa ndani ya tano bora.

Kinara ni Yanga Princess akiwa na jumla ya pointi 38 na mechi zote 14 amecheza bila kupoteza huku Simba ikiwa nayo haijapoteza ila imekusanya sare tatu na Yanga ina sare mbili.
Lema amesema:”Kwetu sisi kila mchezo ni muhimu kusaka pointi tatu na tunajua kwamba ushindani ni mkubwa ila hatuna hofu lazima tupambane.

“Nilikuwa kwenye mchezo wa Simba Queens dhidi ya JKT Tanzania sikuwa na maana yoyote ile zaidi ya kufuatilia mchezo huo kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwenye mechi zingine hivyo tukikutana uwanjani itakuwa mwendo wa kazi,” .
Kibindoni Simba ambao ni mabingwa watetezi wamejikusanyia pointi 36 hivyo tofauti yao ni pointi mbili.


Mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Simba Mo Arena dakika 90, ubao ulisoma Simba Queens 0-0 Yanga Princess jambo lililowafanya wagawane pointi mojamoja.


Mzunguko wa pili mchezo wao utachezwa kesho, Machi 5, Uwanja wa Uhuru, majira ya saa 10:00.


Mussa Mgosi, Kocha Mkuu wa Simba Queens amesema kuwa vijana wake wapo tayari na watapambana kusaka ushindi.

“Wachezaji wangu nimewaandaa vizuri na wanatambua kwamba nini wanakihitaji ndani ya uwanja, utachezwa mpira mwingi kwa kuwa tunakutana na wapinzani wetu ambao wanaongoza ligi.

“Tunawaheshimu na nimewaambia wachezaji kwamba ni lazima kucheza vizuri na kwa tahadhari kwani ligi ina ushindani mkubwa tofauti na msimu uliopita,” .

SOMA NA HII  MGUNDA SIMBA TUNAUTAKA UBINGWA LIGI KUU..."POINTI TULIZOPITWA NI CHACHE SANA..."HAIJAISHA MPAKA IWE IMEISHA KABISA