KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa ni lazima kwa kila mchezaji ambaye ameitwa kwenye timu hiyo kujituma ili kuipa matokeo chanya timu hiyo.
Stars inatarajiwa kuingia kambini Machi 8 ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kufuzu Afcon ambapo ina mechi mbili za kucheza ni ile dhidi ya Eguatorial Guinea itachezwa Machi 25 na Libya itakuwa Machi 28.
Poulsen amesema kuwa wachezaji wengi wana uwezo mkubwa ila wanashindwa kuutumia wote ndani ya uwanja jambo linalofanya matokeo yasiwe mazuri.
“Kuna wachezaji wengi ambao nimewaona na wana uwezo mkubwa ila wamekuwa wakishindwa kuutumia wote. Imefika wakati ambapo wachezaji wanatakiwa kujituma mwanzo mwisho ili kupata matokeo chanya.
“Suala la kushindwa kupata matokeo ugenini hili linasumbua na sio la kufurahisha hivyo ni jukumu la wachezaji kuweza kuwa sawa na kufanya kitu kizuri zaidi ndani ya uwanja,” amesema.
Machi 15 na 18 kikosi cha Stars kinatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Kenya ili kuweza kujenga hali ya kujiamini.
Chanzo:Championi