Home kimataifa GWIJI PELE APEWA KINGA YA CORONA

GWIJI PELE APEWA KINGA YA CORONA


 GWIJI wa soka duniani Edson Arantez do Nascrimento maarufu kama ‘Pele’ amekuwa miongoni mwa Wabrazil wa kwanza kupewa kinga ya maradhi ya Corona.


Pele nyota wa zamani wa soka Brazil ambaye pia ni mshindi wa kombe la dunia mara 3, akitwaa mwaka 1958, 1962 na 1970 mwenye rekodi nyingi nzuri za kuvutia, amekuwa akisumbuliwa na maradhi, mbalimbali tangu kustaafu kwake soka.

 

 ” Najiona mwenye bahati sana kupata kinga hii maana maradhi haya Corona bado yapo duniani na ni janga kubwa sana”, Pele aliandika katika mitandao yake ya kijamii.

 

 

Taifa la Brazil ni moja ya mataifa ambayo yaliathirika sana na janga la Corona tangu kuanza mwishoni mwa mwaka 2019 ambapo rekodi zilizopo zinaonyesha nchi hiyo iliripotiwa kuwa maambukizi ya watu milioni 10.6 na vifo 260,000.

 

 

Pele amepewa kipaumbele cha kupewa kinga hiyo kutokana na heshima ambayo Taifa hilo linampa kama shujaa wao, ni mchezaji aliyoitangaza vyema nchi hiyo wakati akicheza soka, hivyo wanalazimika kumlinda hasa kutokana na umri wake kuwa mkubwa wa miaka 80 kwa sasa.

 

 

Wadau mbalimbali wanaamini Pele na Maradona ndiyo wachezaji wenye vipaji vya juu katika soka kuwahi kutokea duniani hasa katika karne ya 20.

 

 

Takwimu zinaonyesha Pele alifunga magoli 1,279 katika michezo 1,363 aliyocheza ikiwemo ile ya kirafiki kwa mujibu wa kitabu cha kumbukumbu za dunia ‘Guinness’ katika maisha yake kama mchezaji, ikiwemo magoli 77 aliyoifungia timu yake ya Taifa katika michezo 92.


SOMA NA HII  KIPIGO KUTOKA REAL MADRID CHAMVURUGA GUARDIOLA...AGOMA KUZUNGUMZA NA WACHEZAJI WAKE....