Home Yanga SC KOCHA SIMBA :- YANGA BADO INANAFASI YA KUSHINDA UBINGWA LIGI KUU

KOCHA SIMBA :- YANGA BADO INANAFASI YA KUSHINDA UBINGWA LIGI KUU


Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba na sasa ni Mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi amesema bado nafasi ya ubingwa kwa timu hiyo ipo.

Yanga inapewa presha ya ubingwa na watani zao wa jadi, Simba ambayo inahitaji ushindi kwenye mechi mbili ikiwamo ile ya kesho ili kukalia usukani kwenye msimamo wa Ligi.

Simba ni ya pili ikiwa na pointi 45 na mechi nne zaidi mkononi, wakati Yanga iko kileleni ikiwa na pointi 50.

Tayari uongozi wa klabu hiyo umetangaza kuachana na kocha mkuu, Cedrick Kaze na kuvunja benchi lote la ufundi kutokana na mwenendo wa timu hiyo ambayo hivi karibuni ilifungwa na Coastal Union mjini Tanga ikiwa ni kipigo cha kwanza kwenye Ligi kwa kocha Kaze na jana Jumapili imetoka sare na Polisi Tanzania jijini Arusha.

“Bado Kaze hakuwa na mwenendo mbaya kwenye Ligi,” amesema Madadi aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Simba na sasa ni mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Amesema pamoja na Yanga kuachana na kocha Kaze, mrithi wake anatakiwa kujua nguvu ya timu yake ikoje kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa.

“Bado wanayo nafasi, mechi 11 au 15 za Simba kwenye Ligi ya sasa ni nyingi mno, hakuna timu iliyojihakikishia ubingwa, Yanga bado wana fursa hiyo kama watajipanga,” amesema.

Amesema kilichopo ni mrithi wa Kaze kutambua uwezo wa timu yake, kujiandaa kama timu ili ikaweza kuwa na ‘aproch’ tofauti tofauti kulingana na mechi na mechi.

“Huwezi kutegemea kukimbia halafu uchukue ubingwa, lazima uwe na uwezo kumiriki mpira na ukimiriki usikutese, Ligi ya sasa hakuna timu ya kuibeza, kilichopo ni kupambana,”.

Amesema Yanga inahitaji kujenga timu yenye uwezo zaidi uwanjani kuliko kutegemea kushangiliwa.

“Sina uhakika kama walifanya skauti ya kutosha wakati wa usajili wao ambayo ingewapa jibu ya aina ya mchezaji unayemleta, anakuja kufanya nini, anafanya kazi na nani na falsafa ya klabu ni nini?

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA KMC ...GAMONDI APANIA 'MKAZO' KWA MABEKI YANGA....

“Hata hivyo ubingwa wa msimu huu bado uko wazi wachezaji wa Yanga wanahitaji kutengenezwa ili wacheze kama timu kutokana na Ligi yetu pia watambue tageti ya yanga ni nini kwenye msimu, pia wawe na uwezo wa kukabiriana na timu yoyote ile, wakifanikiwa katika hili ubingwa huko wazi bado kwao,” alisema.

Yanga imeusotea ubingwa kwa misimu kadhaa mfululizo huku Simba ikitwaa mara tatu mfululizo mpaka sasa ambapo ni bingwa mtetezi.