BAADA ya mabosi wa Yanga kumfuta kazi Cedric Kaze, nyota wa timu hiyo Tonombe Mukoko amesema kuwa bado wachezaji wana kazi ya kufanya ili kuweza kurejesha hali ya ushindi ndani ya timu.
Kaze amefutwa kazi Machi 7 na kocha wake msaidizi Nizar Khalfan kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo mzunguko wa pili.
Jana Machi 11 Kaze aliwaaga wachezaji wake ambao walionekana wakibubujikwa na machozi kutokana na kocha huyo kutimuliwa akiwa bado hajatimiza malengo yake ya kuwapa ubingwa.
Mukoko ambaye jina lake limetajwa kwenye majina ya wachezaji wa timu ya taifa ya DR Congo amesema kuwa wachezaji pia wana kazi ya kufanya kutimiza majukumu yao kwa ajili ya kuokoa nafasi ya kocha.
“Ikiwa timu inashindwa kupaya matokeo mazuri lawama inakuwa kwa kocha. Lakini na wachezaji pia wana kazi ya kufanya hasa kwa kujituma ndani ya uwanja.
“Wakati wetu ni sasa kutimiza majukumu yetu na kufanya kazi kwa ushirikiano itafanya hata kocha ambaye ataletwa asiwe na kazi kubwa ya kutimiza majukumu yetu,” .