Home Simba SC KOCHA WA SIMBA AWABADILISHIA MBINU AL MERRIKH KWA MKAPA

KOCHA WA SIMBA AWABADILISHIA MBINU AL MERRIKH KWA MKAPA

 


KOCHA wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa mchezo wao wa marudiano na Al Merrikh kuna haja ya kubadili kila kitu ndani ya uwanja ili kuweka mazingira bora ya kuweza kupata pointi tatu.

 

Gomes amesema maandalizi ambayo anayafanya yana utofauti kwani hata wachezaji ambao walitumika kwenye mchezo wa kwanza wanatakiwa kuongezewa nguvu ya wachezaji wengine ambao walikuwa nje ya uwanja kwa kuwa waliona udhaifu wa Al Merrikh kwa uzuri zaidi.


 Gomes amesema, kuna mbinu mbadala ambazo zinatakiwa kutumika ndani ya uwanja kwa sababu wachezaji wa Al Merrikh wana nguvu kubwa na kasi hivyo wachezaji wake watatakiwa kuanza mashambulizi kuanzia nyuma na kwenda mbele huku wakiwa na nidhamu kubwa ya ukabaji.

 

“Huo ni mchezo muhimu sana kwetu kwa sababu ndiyo utarahisisha kazi yetu ya kwenda kucheza kwenye hatua inayofuta, Al Merrikh kila mmoja aliwaona namna ambavyo wanacheza kwa kasi na nguvu kubwa, timu yangu inatakiwa ilitambue hilo.


“Bahati kwamba kila mmoja anatambua umuhimu wa kupata pointi tatu kwenye mchezo huo. Tutaongeza nguvu ya kucheza kuanzia nyuma kwenda mbele na bila shaka tutafanikiwa,” amesema Gomes.

 

Simba walitoka suluhu kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Al Merrikh, na Jumanne ijayo watakutana tena kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa jijini Dar, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.


Mchezo huo utachezwa bila ya uwepo wa mashabiki kutokana na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kutoa zuio hilo.


Kwenye mchezo wao uliopita wa makundi dhidi ya Al Ahly waliweza kushinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Luis Miquissone mashabiki walipata fursa ya kuona mchezo huo na kuipa sapoti timu hiyo ambayo inaongoza kundi A ikiwa na pointi 7.


SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUILALAMIKIA SIMBA KWA KUISUSA MECHI YA LEO...AHMED ALLY KAWAJIBU HAYA KIBABE...