Uncategorized

SIMBA YASHANGAZWA NA UWEPO WA KICHUYA ARDHI YA BONGO

admin August 13, 2019 8:34 am


PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anashangazwa na taarifa ambazo zinaeleza kuwa winga machachari fundi wa kutumia mguu wa kushoto yupoyupo Bongo kwa sasa na hana timu ya kucheza.

Kichuya alisajiliwa na timu ya Pharco ya nchini Misri kwa kandarasi iliyoelezwa ni ya miaka miwili kabla ya kutolewa kwa mkopo ndani ya timu ya ENPPI na alirejea Bongo kwa ajili ya michuano ya Afcon kabla ya kutemwa mazima kikosini.

Aussems amesema :”Sijui kama Kichuya yupo Bongo na kama yupo hapa sijui nini anakifanya kwa sababu kitu ambacho ninakijua mimi yupo nchini Misri ambapo amepata timu na amesaini kandaarasi ya miaka miwili,” amesema.

Kichuya kwa sasa yupo Bongo baada ya mkataba wake mfupi wa miezi sita kuisha na bado hajapata timu alikuwepo kwenye jukwaa la mashabiki siku Simba ilipocheza na Power Dynamo Uwanja wa Taifa.

KOCHA YANGA APANIA KUUFIKISHA MUZIKI KIMATAIFA WAWILI WADAI MILIONI 58 YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply