Uncategorized

KOCHA YANGA APANIA KUUFIKISHA MUZIKI KIMATAIFA

admin August 13, 2019 7:34 am


JUMA Pondamali, aliyekuwa kocha wa makipa ndani ya Yanga amesema kuwa kwa sasa atapambana na muziki kuufikisha hatua za kimataifa.

Pondamali kwa sasa amekacha kazi ya mpira na badala yake amegeukia muziki akiwa ni msimamizi, mwandishi na mwimbaji.

Akizungumza na Saleh Jembe, Pondamali amesema kuwa amefanya uchunguzi wa kutosha na kuona kwamba muziki una nafasi kubwa ya kumtoa kwenye maisha.

“Naifanya hii kazi haimanishi nimeanza leo nimeanza muda mrefu sana na nimetunga nyimbo nyingi za Yanga ambazo hazikupata umaarufu mkubwa kutokana na kutokuwepo na matamasha kama ambavyo wapinzani wetu walikuwa wanafanya.

“Muziki ambao nasimamia na kufanya ni Singile huku ndiko ambako nitafiti hivyo mipango mingi inakuja na nyimbo kali zinakuja, lengo kubwa ni kuvuka hatua ya kitaifa mpaka kimataifa” amesema.

YANGA YAENDA CHIMBO KUTAFUTA DAWA YA TOWNSHIP ROLLERS SIMBA YASHANGAZWA NA UWEPO WA KICHUYA ARDHI YA BONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply