Namungo FC

PAMBA JIJI YAZOA BEKI NAMUNGO

Vardo May 30, 2026 9:39 am

PAMBA Jiji imeshamalizana na beki wa kushoto wa Namungo, Salehe Machupa, huku klabu hiyo ikimpa baraka zote.

Kiwango cha beki huyo kiliwakosha mabosi Pamba ambayo wapo kwenye nafasi ya saba katika msimamo wa ligi, ikiwa imecheza mechi 25, imeshinda nane na kupoteza nane na sare tisa ikifikisha jumla ya pointi 33.

Akizungumza na Soka la Bongo, Katibu wa Namungo, Ally Suleiman amesema klabu hiyo ilimsajili beki huyo msimu uliopita kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Amesema kuwa, Machupa hajasema chochote kwa uongozi wa kikosi hicho na wao pia wanasikia tu taarifa kwenye mitandao ya kijamii, kwa hiyo wanasubiri kama hilo litatokea.

“Sio kweli kama ana mkataba zaidi, ila kama mchezaji akitaka kutafuta changamoto mpya na mkataba wake unamalizika basi hakuna shida na mimi kama katibu namtakia kila la kheri tu. “Tumesalia na mechi tano tumalize ligi na ushindani ni mkubwa nadhani jambo la msingi ni kupambana kipindi hiki cha likizo fupi, timu inakuja Dar Jumatatu tutakuwa na mazoezi ya kuendelea kujinoa ili tumalize vyema,” amesema.

Kisheria mchezaji anakuwa huru kuanza mazungumzo na timu nyingine endapo mkataba wake utakuwa umesalia miezi sita kumalizika, hivyo alichokifanya Machupa ni sahihi.

Mchezo unaofuata Juni 12, 2026, Namungo itakutana na Coastal Union ugenini kusaka alama tatu za kujikwamua kwenye hatari ya kushuka daraja, huku kwa sasa ikiwa nafasi ya 13 ikifikisha pointi 27.

ULE UTAMU WA CHAMPIONSHIP SASA UMEFIKIA PAZURI SEIF KARIHE AFICHUA JAMBO MASHUJAA