Mlandege FC Yafanya Mabadiliko Makubwa: Yatemema Nyota 18 Msimu wa 2026/27
Klabu ya Mlandege inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar (PBZ Premier League) imechukua hatua nzito ya kusuka upya kikosi chake kuelekea msimu ujao wa 2026-2027, baada ya kutangaza rasmi kuachana na wachezaji 18.
Mabadiliko haya makubwa yanakuja ikiwa ni mkakati wa klabu hiyo kurejesha makali yake, kufuatia kumaliza katika nafasi ya nne msimu wa 2025-2026—baada ya kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Zanzibar msimu wa 2024-2025.
Wachezaji walioachwa na Mlandege FC:
Wachezaji waliotishiwa mkataba na kupewa mkono wa kwaheri ni pamoja na:
-
Abuubakar Hussein Ali
-
David John Chiwalanga
-
Fasbir Sabri Ramadhan
-
Hamad Ubwa Hamad ‘Baro’
-
Ibrahim Samwel Tuvan
-
Lucas Sadock Ntikahela
-
Mussa Hassan Salum
-
Nonyem Emmanuel Okorocha
-
Qassim Nassour Hilal
-
Ramadhan Mzee Kiparamoto
-
Said Mussa Said
-
Said Suleiman Othman
-
Salum Suleiman Salum
-
Sospeter Maiko Chikande
-
Yusuf Jamal Khamis
Hatua Mpya za Nyota Hao
Baadhi ya wachezaji hao tayari wameshapata hifadhi mpya katika klabu mbalimbali:
-
Hamad Ubwa ‘Baro’ na Said Mussa Mbeki wamejiunga na KVZ FC.
-
Mussa Hassan Simba ‘Mbappe’ ametua Singida Black Stars (Tanzania Bara).
-
Nonyem Emanuel ‘Okorocha’ yeye amejiunga na Pamba Jiji FC.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Uongozi wa Mlandege FC, klabu hiyo imewashukuru wachezaji hao kwa mchango wao mkubwa:
“Tunawaaga lakini mtaendelea kubaki sehemu ya familia ya Mlandege. Tunawatakia kila la kheri na mafanikio mema katika hatua mpya za kazi zenu za soka,” ilieleza taarifa hiyo.
Mlandege inaingia sokoni kusajili majina mapya yenye uwezo wa kurudisha heshima na klabu hiyo kuwania tena ubingwa msimu ujao.