HUBERT Velud, raia wa Ufaransa inaelezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na baadhi ya mabosi wa Yanga wakiwa na mpango wa kumpa dili la kukinoa kikosi hicho ambacho kwa sasa kipo chini ya Kaimu Kocha, Juma Mwambusi.
Amewahi kuwa Kocha Mkuu wa TP Mazembe msimu wa 2016, Etoile Sportive du Sajel msimu wa 2017, pia USM Alger na ES Setif jambo linalowapa nguvu viongozi wa timu hiyo kumpa mkataba.
Raia huyo wa Ufaransa ambaye nafasi aliyokuwa anacheza ilikuwa ni kipa anapewa chapuo la kuwa mrithi wa Kaze.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa utaratibu wa kumpata mrithi wa Kaze unafanyika na hivi karibuni atatambulishwa kwa mashabiki.
“Kila kitu kuhusu kumpata mrithi wa Kaze kipo sawa na ipo kamati ambayo inashughulikia masuala ya upatikanaji wa kocha, huko CV zitatumwa na mchakato utafanyika kupitia kamati ya utendaji,” .