Simba SC

SIMBA WAMFUATA BEKI HUYU KITASA WAMPE DILI

admin March 15, 2021 6:47 am

 


BEKI wa kulia wa AS Vita, Djuma Shabani amekiri kuwa ni kweli alifuatwa na viongozi wa Simba ili kuangalia uwezekano wa kujiunga nao mwishoni mwa msimu.

Djuma amekuwa katika kiwango bora ndani ya AS Vita ambapo msimu huu katika michuano yote aliyoichezea timu hiyo amefunga mabao 6 na kutoa pasi tano za mabao.

Akizungumzia uwezekano wa kutua Simba Djuma amesema: “Ni kweli kuna baadhi ya viongozi wa Simba walinitafuta kwa ajili ya mazungumzo ya awali ya usajili lakini siwezi kulizungumzia sana hilo kwa sasa.

“Hii ni kwa sababu wote kwa sasa tunapambana kuzisaidia timu zetu zifanye vizuri katika michuano ya kimataifa ikizingatiwa tupo kundi moja, ” .

Ikiwa nyota huyo atamalizana na mabosi wa Simba atakwenda kuongeza nguvu upande wa beki wa kulia na kusaidiana na Shomari Kapombe ambaye ni chaguo namba moja la Didier Gomes.  



TOTTENHAM YACHAPWA NA ARSENAL, LAMELA APIGA BONGE MOJA YA BAO KAZE :- SHIDA KUBWA YA YANGA NI UWEPO WA ”MABABA WAWILI” WENYE KAULI SAWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply