UONGOZI wa klabu ya Azam inayomiliki uwanja wa Azam Complex, ambao umekuwa ukitumiwa na Namungo kwa ajili ya michezo ya kimataifa umesema kuwa, bado unaendelea kufuatilia sababu za uwanja huo kuzuiwa kutumika kwenye michezo ya kimataifa wakati tayari ulikuwa na kibali.
Namungo imelazimika kucheza mchezo wake wa leo dhidi ya Pyramids ya Misri katika dimba la Mkapa, badala ya Azam Complex kutokana na zuio hilo.
Akizungumzia sakata hilo Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam amesema: “Tunaendelea kufuatilia kama kuna mabadiliko yoyote ya vigezo vya uwanja unaopaswa kutumiwa kwa ajili ya michuano ya kimataiafa.
“Tunafanya hivi ili kuona kama kuna mapungufu yoyote basi turekebishe, maana tayari uwanja huu ulikuwa na ruhusa ya kutumika kwa michezo ya kimataifa,”