Ligi Kuu

DIDA MAMBO MAGUMU IHEFU, KOCHA ATOA NENO LA MATUMAINI

admin March 19, 2021 12:47 pm


KAZI inaonekana kuwa nzito kwa kipa namba moja wa Klabu ya Ihefu FC, Deogratius Munish, ‘Dida’ kwenye kulinda ngome yake kwa kuwa amekuwa akitunguliwa kwenye mechi zake uwanjani.

Akiwa ni ingizo jipya dirisha dogo la Januari akiwa ni mchezaji huru amekaa langoni kwenye jumla ya mechi 9 na ameokota nyavuni jumla ya mabao 15.

Timu yake jumla imeruhusu mabao 34 baada ya kucheza mechi 24 hivyo inaonesha kuwa safu ya ulinzi ya Ihefu inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila bado haijawa kwenye ubora.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 17 imekusanya pointi 20 kwa msimu wa 2020/21.

Katwila amesema kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zilizobaki.

“Bado kuna mechi ambazo zipo hizo tutazitumia kwa ajili ya kuendelea kupata matokeo chanya hivyo mashabiki watupe sapoti,” .

MAMA SAMIA AAPISHWA KUWA RAIS WA TANZANIA – VIDEO ZIMBWE JR AWEKA REKODI YAKE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply