KLABU ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes mkononi kwa sasa ina mechi mbili za kukamilisha kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Inahitaji pointi moja ili kuweza kufikisha pointi 11 ambazo zitaifanya iweze kutinga hatua ya robo fainali.
Ikiwa kundi A inaongoza ikiwa na pointi 10 inafuatiwa na Al Ahly yenye pointi 7, AS Vita ni ya tatu na pointi nne huku Al Merrikh ikiwa nafasi ya nne na pointi moja.
Mechi zake mbili moja inatarajiwa kuchezwa Machi 3 Uwanja wa Mkapa ni Simba v AS Vita ya Congo ambapo mchezo wa kwanza walipokutana nchini Congo, Simba ilishinda bao 1-0.
Bao pekee lililoipa pointi tatu Simba lilifungwa na Chris Mugalu kwa mkwaju wa penalti baada ya Luis Miquissone kuchezewa faulo ndani ya 18.
Itakutana na Al Ahly Aprili 9, nchini Misri, Uwanja wa Taifa wa Cairo. Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda bao 1-0 na kusepa na pointi zote sita kwa Mkapa.
Gomes amesema kuwa mechi mbili zilizobaki ni muhimu na anahitaji kuona wachezaji wake wakipambana kupata ushindi.
“Tunahitaji pointi moja kutinga hatua ya robo fainali ila haitakuwa rahisi kwa kuwa mechi zote zina ushindani mkubwa na kila timu inahitaji ushindi,” .