Home Azam FC AZAM FC: MAGUFULI ALIKUWA KIONGOZI IMARA MWENYE MAAMUZI

AZAM FC: MAGUFULI ALIKUWA KIONGOZI IMARA MWENYE MAAMUZI


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kuondoka kwa Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli ni pigo kwa Tanzania na Afrika kwa kuwa ameondoka kiongozi shujaa aliyekuwa ni mpenda michezo na mtu wa maamuzi.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kwa bara la Afrika, Magufuli aliweka rekodi ya kuruhusu mashabiki na mechi kuanza kufanyika mapema wakati wa janga la virusi vya Corona.

Wakati Corona ikitikisa dunia 2020, nchi nyingi Afrika na duniani ziliweka zuio kwenye masuala yote yanayohusu michezo na mikusanyiko ila Magufuli hakuwa tayari kuona hilo likiwa endelevu kwa muda mrefu jambo ambalo Azam FC na Afrika linatambua.

Thabit amesema:”Alikuwa kiongozi imara, shupavu na mwenye msimamo, ikumbukwe kwamba Tanzania chini ya utawala wake wakati wa changamoto ya Corona, aliruhusu soka kuendelea.

“Ilikuwa ni kuanzia Julai Mosi ambapo aliruhusu masuala ya michezo kuendelea na mashabiki pia kuingia kwa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona, ni alama ambayo ameiacha na atakumbukwa daima,” .

Magufuli alikuwa ni mpenda maendeleo na alikuwa na ushirikiano na viongozi wengi ndani ya bara la Afrika na nje ya Afrika ambapo kwenye kutoa heshima zao za mwisho wengi jana Machi 22 walijitokeza makao makuu ya Tanzania, Dodoma.

Miongoni mwa wale ambao walikuwa kwenye kutoa heshima za mwisho ni pamoja na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata ambaye aliweka wazi kuwa Magufuli alikuwa muongoza njia na mpenda maendeleo.

“Magufuli alikuwa muongoza njia na katika hayo alikuwa anapenda kuona maendeleo yakionekana, hivyo kuondoka kwake ni pengo, tutamkubuka,” .


SOMA NA HII  AZAM FC KAZINI TENA LEO KOMBE LA KAGAME