MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Abdulazack amesema kuwa Afrika imepata pigo pamoja na Tanzania kwa kuondokewa na kiongozi shujaa, Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli.
Magufuli alitangulia mbele za haki, Machi 17 kwa mujibu wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu ambaye kwa sasa kwa mujibu wa katiba ya Tanzania ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Fiston ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga zama zile za kocha Cedric Kaze ambaye amefutwa kazi Machi 7 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu ya timu hiyo yupo ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kinanolewa na Juma Mwambusi ambaye ni kaimu.
Nyota huyo ambaye alifunga bao lake la kwanza mbele ya Polisi Tanzania wakati Yanga ikigawana pointi mojamoja na timu hiyo Uwanja wa Sheikh Amri Abeidkwa kufungana bao 1-1 amesema kuwa ni pigo kwa Tanzania.
“Ni pigo kwa Tanzania na Afrika kiujumla kwa kuwa ambaye ameondoka ni kiongozi wa watu, alikuwa mchapakazi na atakumbukwa kwa kupenda watu wake daima.
“Imani yetu ni kwamba mwendo ameumaliza hivyo wakati uliobaki kwa sasa ni kumuombea apumzike salama shujaa wa Afrika,” .