Home Yanga SC HUYU HAPA MFARANSA MRITHI WA MIKOBA YA KAZE YANGA

HUYU HAPA MFARANSA MRITHI WA MIKOBA YA KAZE YANGA


 BAADA ya Cedric Kaze aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, kufutwa kazi Machi 7 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu, Mfaransa Sebastian Migne anatajwa kuwasili Bongo kuchukua mikoba yake.


Kaze alitoa Bongo kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye alifutwa kazi baada ya kuongoza mechi tano za Ligi Kuu Bara,  alishinda nne na sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons,  Uwanja wa Mkapa.


Kaze mzunguko wa pili mambo yalikuwa magumu kwake ambapo katika mechi 6, alishinda moja, sare nne na alipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 mbele ya Coastal Union,  Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


Kaze alitua Bongo, Oktoba 15,2020 na mchezo wake wa Kwanza ilikuwa Uwanja wa Uhuru dhidi ya Polisi Tanzania timu yake ikishinda bao 1-0 na mchezo wake wa mwisho ilikuwa dhidi ya Polisi Tanzania,  Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,  alishuhudia ubao ukisoma Polisi Tanzania 1-1 Yanga.

SOMA NA HII  MUDATHIR:- BAO LILIANZIA BENCHI...