Home Azam FC AZAM FC KAMILI GADO, YAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

AZAM FC KAMILI GADO, YAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR


 VIVIER Bahati, kocha msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wanatambua kwamba mchezo wao wa leo dhidi ya Kagera Sugar utakuwa mgumu ila wapo tayari kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu.

Ikiwa imejichimbia nafasi ya tatu na pointi zake ni 37 inakutana na Kagera Sugar ambayo ipo nafasi ya 10 na pointi zake kibindoni ni 24 na zote zimecheza jumla ya mechi 21.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Aam Complex, Azam FC ilishinda kwa mabao 4-2 na ulikuwa ni mchezo wa kwanza kukusanya mabao mengi ndani ya uwanja kwa mzunguko wa kwanza kabla ya ule  wa Coastal Union 0-7 Simba.

Vivier amesema:”Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa kwa sababu tunacheza na timu bora na imara.

“Hivyo tutajitahidi kucheza katika ubora wa hali ya juu ili kupata matokeo chanya, mashabiki watupe sapoti katika hili”.

Mecky Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa amewaambia vijana wake wafanye kazi ya kusaka pointi tatu hivyo mashabiki wajitokeze kuwapa sapoti ndani ya Kaitaba.

Mabao hayo mawili ambayo Kagera Sugar walifunga walimtungua kipa namba moja David Kissu ambapo kwa sasa amekuwa akisugua benchi na nafasi yake ipo mikononi mwa Martin Kigonya.

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA MSIMU HUU..DUBE AMCHIMBA MKWARA MAYELE...