Home Azam FC AZAM FC KUWAKOSA WADADA NA SEBO

AZAM FC KUWAKOSA WADADA NA SEBO


KLABU ya Azam leo katika mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC itawakosa nyota wake wawili Nicolas Wadada na Abdallah Kheri ‘Sebo’.

Wadada aliumia katika mazoezi ya mwisho wakijiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Sebo yeye aliumia katika mchezo wao na Kagera Sugar.

Azam tayari ilishawasili Shinyanga, Machi 4 wakitokea Bukoba kwa usafiri wa ndege wakishuka Mwanza na kusafiri kwa gari mpaka Shinyanga.

Baada ya kufika walifanya mazoezi katika uwanja wa Fresh Complex, jana jioni walifanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Mwadui Complex saa 10:00 jioni.

Mchezo wa Mwadui na Azam utachezwa leo saa 10:00 jioni katika uwanja wa Mwadui Complex, huku Azam FC wakiwa na morali ya ushindi baada ya kuifunga Kagera Sugar 2-1 huku Mwadui wakifungwa 1-0 na Namungo.

KIGONYA AITWA THE CRANES

Wakatiu huo huo kipa wa Azam FC, Mathias Kigonya ameitwa kwenye kikosi cha The Cranes, kwa ajili ya michezo ya kufuzu AFCON dhidi ya Burkina Faso na Malawi.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwake tangu 2016 aliposhiriki CHAN.

SOMA NA HII  KUHUSU MANULA KURUDI AZAM...JAMBO LINAPIKWA KIMYA KIMYA AISEE...