Home Simba SC GOMES WA SIMBA AWAPA TAHADHARI WACHEZAJI WAKE MAPEMA KIMATAIFA

GOMES WA SIMBA AWAPA TAHADHARI WACHEZAJI WAKE MAPEMA KIMATAIFA


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa mchezo wao dhidi ya AS Vita utakuwa na ushindani mkubwa jambo ambalo analitambua na amewaambia wachezaji wake.

Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ipo hatua ya makundi inaongoza kundi A na pointi zake 10 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya AS Vita, Aprili 3 Uwanja wa Mkapa.

AS Vita kwenye kundi A ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 4 inahitaji kufufua matumaini ya kusonga mbele na kutinga hatua ya makundi kama ilivyo kwa Simba jambo ambalo litaongeza ugumu kwenye mchezo huo.

Gomes amesema:”Nimewaambia wachezaji kwamba haitakuwa kazi nyepesi kwetu na kila timu inahitaji ushindi hivyo ni muhimu kujipanga vizuri.

“Ikiwa tutashindwa kupata matokeo itakuwa ngumu kwetu kufikia malengo ya hatua ya robo fainali hivyo tupo tayari kufanya vizuri,” .

SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA KESHO MWISHO WA UBABE....SHOW YOTE KUPIGWA UHURU MCHANA KWEUPEE..