Home Ligi Kuu MAKOCHA 15 WAJITOKEZA KUOMBA KAZI BIASHARA UNITED

MAKOCHA 15 WAJITOKEZA KUOMBA KAZI BIASHARA UNITED


 UONGOZI wa Biashara United umeweka wazi kuwa umepokea majina zaidi ya 15 ya makocha ambao wanaomba kazi ya kukinoa kikosi hicho chenye maskani yake Mara.

Kwa sasa Biashara United ipo mikononi mwa Marocha Mbili ambaye ni Kaimu Kocha Mkuu wa muda mpaka pale atakapopatikana kocha mpya.

Aliyekuwa kocha wa Biashara United, Francis Baraza aesepa ndani ya timu hiyo na kuibukia ndani ya Kagera Sugar akichukua mikoba ya Mecky Maxime ambaye alifutwa kazi kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo.

Mwenyekiti wa Biashara United, Seleman Mataso amesema kuwa mchakato wa kumsaka kocha mpya unaendelea na wapo ambao wametuma maombi kukinoa kikosi chetu.

“Kuna majina ya makocha zaidi ya 10 ambao wameomba kazi kukinoa kikosi chetu hivyo mchakato unaendelea hivyo muhimu kwetu kwa sasa ni kuangalia wale ambao watakidhi vigezo vya kuinoa timu yetu.

“Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi lakini nasi pia tutaonyesha ushindani ili kupata matokeo bora,” .

SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA HUYU HAPA, NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI