Home Azam FC IDD NADO AMEWAKA HATARI

IDD NADO AMEWAKA HATARI


BAADA ya Alhamisi iliyopita kufunga mabao mawili na kuasisti bao moja kwenye ushindi wa mabao 3-0 walioupata Azam dhidi ya klabu ya Ihefu, kiungo mshambuliaji wa Azam, Idd Selemani Nado ‘Idd Nado’ sasa amehusika kwenye mabao 12 ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Nado sasa anaifukuzia rekodi yake ya kufunga mabao kumi ndani msimu mmoja, akiwa amebakisha mabao matatu pekee.

Msimu huu mpaka sasa, Nado amefunga mabao saba, na kuasisti mara tano.

Nado sasa yupo nyuma ya vinara wa msimamo wa wafungaji, John Bocco na Meddie Kagere wa Simba kwa tofauti ya mabao mawili. Nyota hao wa Simba kila mmoja amefunga mabao tisa.

Akizungumzia kasi yake Nado amesema: “Nafurahi kuwa katika kiwango bora, hii inatokana na kazi kubwa ambayo makocha wangu wamekuwa wakiifanya kunisaidia kukuza kiwango changu.

“Siwezi kusema nitafunga mabao mangapi, lakini naweza kuahidi kufunga kwa kila nafasi ambayo nitakuwa naipata,” 

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YAO YA LIGI....FEI TOTO KAIBUKA NA HILI JIPYA KWA YANGA...