Home Azam FC WAKATI ALEX SONG NA SOLOMON KALOU WAKIKIPIGA NA AZAM….THADEO LWANGA ATAMBULISHWA NDANI...

WAKATI ALEX SONG NA SOLOMON KALOU WAKIKIPIGA NA AZAM….THADEO LWANGA ATAMBULISHWA NDANI YA NYUMBA…


Matajiri wa Chamazi, Azam FC katika kuendelea kujiweka sawa na mashindano ya Ligi Kuu NBC pamoja na Shirikisho Afrika kwa muda huu ligi imeenda mapumziko kwa ajili ya kupisha ratiba ya CAF itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya AS arta Solar 7.

Azam imethibithitisha taarifa hiyo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii “Kikosi chetu kinatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Djibout, AS Arta Solar 7, mechi itakayofanyika Azam Complex Agosti 30 saa 1.00 usiku.”

Arta Solar ni mabingwa wa Ligi Kuu Djibout ikiwa na mastaa waliowahi kuwika katika Ligi Kuu England kama Alex Song raia wa Cameroon na Solomon Kalou wa Ivory coast.

Vilevile timu hiyo imenasa saini ya aliyekuwa kiungo wa Simba, Taddeo Lwanga aliyeachana na Simba mwanzoni mwa mwezi Agosti.

SOMA NA HII  KISA MBINU ANAZOTUMIA PABLO...MGOSI ASHINDWA KUJIZUIA...AIBUKA NA KUFUNGUKA HAYA...