Home epl JOSE MOURINHO MAMBO MAGUMU SPURS

JOSE MOURINHO MAMBO MAGUMU SPURS


JOSE Mourinho jana alishindwa kukiongoza kikosi chake cha Totternham Hotspurs kufuzu hatua ya robo fainali ya Ueropa ligi maarufu kama ‘ UEFA ndogo’.

 

 

Totternham ilikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Dinamo Zagreb ya Croatia katika mechi ya mkondo wa pili, iliyolazimika kwenda kwenye muda wa nyongeza baada ya dakika 90 kumalizika kwa wenyeji kushinda 2-0, na hivyo kufanya kuwa sare ya 2-2 kufuatia mchezo wa kwanza Spurs ilishinda 2-0.

 

 

Baada ya matokeo hayo, mashabiki mbalimbali wameonekana kumnyoshea kidole kocha Jose Mourinho wakimtaka mmiliki wake Daniel Levy kumtimua kwa kuwa hawaoni umuhimu wowote wa kuendelea naye wakiamini zama zake zimefika mwisho.

 

 

Hoja ya mashabiki imekuja baada ya kutathimini mwenendo wa timu hiyo tangu Mourinho alivyoichukua timu hivyo novemba 2019, ushiriki wa ligi na vikombe mbalimbali ikiwemo hiki cha Ueropa ambapo wametolewa jana.


 Katika msimamo wa ligi Spurs ni ya 8 ikiwa na alama 45 na kuzua hofu ya kufuzu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

 Mourinho miongoni mwa makocha bora duniani ambao wamepata mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa kombe la ligi ya mabingwa Ulaya mara 2 akiwa na vilabu vya FC Porto na Inter Milan na pia ubingwa wa ligi kwa baadhi ya timu alizozifundisha kama Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid kwa mwenendo anaokwenda nao katika timu ya Totternham unaashiria kutofanikiwa kabisa.

 

 

Takwimu za Mourinho akiwa na Totternham Hotspurs ambako hadi sasa amekaa kwa takribani miezi 15 ameiongoza timu katika michezo 82, ameshinda michezo 43 sare 17 na kupoteza michezo 22.


SOMA NA HII  ILIKUWA MPANGO WA ARSENAL KUMSAJILI BEN WHITE