Home Simba SC KAGERE BADO ANAWAZA KIATU CHAKE

KAGERE BADO ANAWAZA KIATU CHAKE

 

MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba, amesema bado anaamini ataendelea kufunga mabao kila atakapopata nafasi ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mfungaji bora msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara.

Ikiwa ataweza kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo msimu huu wa 2020/21, Kagere atakuwa ameweka rekodi ya kutwaa tuzo hiyo mara tatu mfululizo kwa kuwa tayari amefanya hivyo msimu wake wa kwanza 2018/19 akitupia mabao 23 na msimu wa 2019/20 alitupia mabao 22.

 Ushindani kwenye kucheka na nyavu msimu huu umekuwa mkubwa ambapo Kagere akiwa na mabao tisa kabla ya mechi ya jana, anayemfuatia ni John Bocco wa Simba mwenye mabao nane, huku Price Dube wa Azam FC, Adam Adam wa JKT Tanzania na Meshack Abraham wa Gwambina, kila mmoja akitupia mabao saba.

 β€œNi msimu wa kipekee ndani ya ligi na kila mchezaji anafanya vizuri, hilo lipo wazi.β€œKwangu ninapambana ili kufunga pale ambapo nitakuwa ninapata nafasi. Malengo ni kuwa mfungaji bora,” alisema Kagere.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA , YANGA WAKIENDELEA KUTANGAZA WACHEZAJI WAKE WAPYA.... WASENEGAL WA AZAM WATAMBA TUNISIA