Home Yanga SC KAZE AKUBALI YAISHE MBELE YA COASTAL

KAZE AKUBALI YAISHE MBELE YA COASTAL

 


KOCHA mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amefunguka kuwa anaipongeza Coastal kwa ushindi walioupata dhidi ya klabu yake siku ya leo, huku pia akiwapongeza nyota wake kwa kupambana.

Yanga leo katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga imepoteza kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1.

Akizungumzia mchezo huo Kaze amesema: “Tulikuwa na mchezo mzuri dhidi ya wapinzani wetu na kufanikiwa kupata penalti mwanzoni, lakini kwa bahati mbaya tuliikosa.

“Lakini nawapongeza vijana wangu kwa kupambana, pamoja na wapinzani wetu kwa ushindi walioupata,”

SOMA NA HII  KUHUSU KUSEPA YANGA...AZIZI KI AVUNJA UKIMYA...AFUNGUKA A-Z 'PLAN' ZAKE ZILIVYO..