Home Simba SC ALICHOSEMA MANARA HUKO SUDAN BAADA YA YANGA SC KUFUNGWA LEO

ALICHOSEMA MANARA HUKO SUDAN BAADA YA YANGA SC KUFUNGWA LEO


SUDAN. BAADA ya kupata habari kuwa Yanga, wapo nyuma kwa mabao 2-1, dhidi ya Coastal Union, Ofisa habari wa Simba, Haji Manara alishindwa kujizuia na kutoa kituko.

Wakati mazoezi ya Simba, yakiendelea kwenye uwanja wa Jeshi la Khartoum, Manara alipewa taarifa na mmoja wa kiongozi wa Simba kuwa Yanga wapo nyuma kwa mabao 2-1.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Manara ambaye alikuwa amekaa chini alisimama na kuuliza mechi imebaki dakika ngapi kabla ya kumalizika.

Alipewa majibu kuwa zimebaki dakika tano, ndio hapo Manara alishindwa kuzuia hisia zake.

Manara alinyanyuka na kuanza kutembea taratibu akizunguka uwanja huo wakati Simba wakiwa aanaendelea na mazoezi.

Baada ya kuzunguka mara ya kwanza kwa hoja aliyoeleza kuwa umeshindwa kujizuia na presha na kuvumilia hizo dakika tano bora atembee uwanja mzima ili zimalizike.

Baada ya kuzunguka awamu ya kwanza walifika hadi eneo walipo wachezaji wa Simba na kumwambia mechi ni mabao 2-2, hapo alishtuka na kuanza kunyong’onyea.

Muda mfupi kabla ya kuambiwa jambo hilo aliambiwa anataniwa na matokeo bado hapo vile vile Coastal 2-1, Yanga ila zimeongezwa dakika tano kabla ya mechi kuisha.

“Siwezi kuvumilia hizi dakika tano, ngoja nitembee tena kwa mara ya pili nizunguke tena uwanja na nikifika hapa mechi uwe imemalizika,” alisema Manara.

Baada ya kuzunguka kwa mara ya pili tena uwanja mzima alifika katika eneo la alilioanza kutembea na mechi kukuta dakika chache kabla ya kumalizika.

Baada ya mechi kumalizika kwa Yanga kufungwa 2-1, na Coastal alionekana kucheza na kufurahi.

“Niache tu wakati huu hawa Coastal wamenifurahisha leo ila mengi zaidi tutaona hapo baadae,” alisema Manara.

SOMA NA HII  DUH...WAWA NDIO BASI TENA SIMBA...'MAJEMBE MAPYA YA MAANA KUTUA'..SABABU HIZI HAPA...