Home Ligi Kuu KIUNGO HASSAN NASORO AIPIGIA HESABU TANO BORA

KIUNGO HASSAN NASORO AIPIGIA HESABU TANO BORA


 HASSAN Nassoro, kiungo mzawa mwenye uwezo wa kupiga pasi ndefu uwanjani amesema kuwa anaamini timu hiyo itamaliza ikiwa ndani ya tano bora.

Nassoro ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Malale Hamsini ambaye ni mzawa anayekinoa kikosi hicho.

Nassoro amesema kuwa ushindani ndani ya ligi ni mkubwa jambo ambalo linawafanya nao wapambane ili wamalize ndani ya tano bora.

“Ipo wazi kwamba kila timu kwa sasa inasaka ushindi hasa ukizingatia huu ni mzunguko wa pili. Kwetu sisi tunahitaji kumaliza ndani ya tano bora na hiyo ni nafasi ambayo tunaihitaji.

“Jambo la msingi ambalo tunalifanya ni kupata matokeo kwenye mechi zetu ambazo tutacheza. Kwani kupata pointi kunahitaji ushindi na hakuna jambo lingine,” amesema.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya 8 ikiwa imecheza mechi 22 imekusanya jumla ya pointi 29, kinara wa ligi ni Yanga ikiwa na pointi 50.

SOMA NA HII  GEITA GOLD:TUNAWAHESHIMU YANGA ILA TUNATAKA POINTI TATU