Home Ligi Kuu KOCHA BARAZA WA BIASHARA UNITED AMTAKA BANDA KIKOSINI

KOCHA BARAZA WA BIASHARA UNITED AMTAKA BANDA KIKOSINI


 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa malamiko ya mchezaji wake Omary Banda kwamba hajalipwa mshahara ndani ya kikosi hicho ni kweli ila bado anahitaji huduma yake.

Nyota huyo hivi karibuni alipeleka malalamiko yake Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kwa kueleza kuwa hajalipwa stahiki zake kwa muda wa miezi mitano.

Pia alieleza kuwa hakupewa huduma baada ya kuumia ndani ya timu hiyo ambayo inashiriki Ligi Kuu Bara.

Baraza amesema:”Ni kweli mchezaji wetu Banda anadai na hajalipwa stahiki zake ila nimeongea na mwenyekiti kuhusu Banda na nimemuomba afanya mpango arudi kwani ni mchezaji mzuri.

“Kuhusu kulipwa ni kweli hata mimi pia bado kuna madai lakini imani ni kwamba nitalipwa, kuhusu malipo mimi sihusiki wenye mamlaka ambao ni viongozi tumeongea watakamilisha,” .

SOMA NA HII  HIZI HAPA KUSHIRIKI LIGI DARAJA LA KWANZA PAMOJA NA ZITAKAZOCHEZA PLAY OFF