Simba imepoteza penalti tatu kati ya nne walizopiga katika michezo yao ya michuano mbalimbali iliyopita, kati ya hizo Chama alikosa dhidi ya Azam Feruari 7 mwaka huu.
Kagere akakosa dhidi ya African Lyon Februari 27, mwaka huu na juzi Jumatano, Chris Mugalu alikosa penalti dhidi ya Tanzania Prisons.
Penalti pekee ambayo Simba wamefanikiwa kufunga ni ile ya Chris Mugalu katika ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya AS Vita ya DR Congo, kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Februari 12, mwaka huu.
Akizungumzia hali hiyo Gomes amesema: “Kuhusu ishu ya kukosa penalti, kwanza nisingependa kuwalaumu wachezaji wangu katika hilo.
“Lakini ni lazima tuhakikishe tunamaliza tatizo hilo kwa kuandaa programu maalum ya mazoezi, ili kuelekeza juu ya upigaji wa mipira ya kutenga hususani penalti, kwa kuwa sitaki kuona tunashindwa kupata matokeo kwa sababu hiyo,”