Home Yanga SC MGHANA YANGA: TUPO FITI ASILIMIA 100

MGHANA YANGA: TUPO FITI ASILIMIA 100


KOCHA wa viungo wa Yanga raia wa Ghana, Edem Mortotsi amesema kuwa kwa kipindi hiki cha mapumziko ya ligi amejikita zaidi kwenye kutengeneza utimamu wa mwili ‘fitness’ kwa wachezaji wake ambao walibaki kambini.

Akizungumzia hali za nyota wa kikosi hicho Mortotsi amesema wakati anakuja kwenye kikosi hicho alikuta baadhi ya wachezaji fitness yao ikiwa ya kawaida, hivyo jambo la kwanza alilofanya ni kuhakikisha wachezaji wote wanakuwa kwenye levo moja ya fitness jambo ambalo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Namshukuru Mungu kuwa kila kitu kinakwenda vizuri sana kwa upande wa wachezaji wangu, ukitazama utimamu wao wa mwili kwa sasa nitofauti na ilivyokuwa mwanzo.

“Kwa sasa wachezaji wote wameonyesha kuongezeka fitness jambo ambalo nilikuwa nalihitaji kuliona likifanikiwa wakati nilipofika kwenye timu hii,” alisema Edem.

Yanga ipo kwenye kambi yao Kigamboni Avic ikiendelea na maandalizi yao ya kumalizia michezo kadhaa ya ligi kuu chini ya kocha wa muda Juma Mwambusi.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA USAJILI WA PHIRI...MWAKALEBELA AAMUA KUIWAHI SIMBA ...AGUSIA MCHEZO MZIMA ULIVYO...