Home Ligi Kuu MTIBWA SUGAR HAWAJASHIDA TANGU MWAKA JANA MJUE

MTIBWA SUGAR HAWAJASHIDA TANGU MWAKA JANA MJUE


TAARIFA ikufikie kuwa, kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar hakijashinda mchezo wowote wa ligi kuu tangu kuanza kwa mwaka 2021.

Mara ya mwisho kwa Mtibwa kupata ushindi ilikuwa ni Desemba 19, 2020 walipowafunga JKT Tanzania kwa bao 1-0 mchezo ukichezwa uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Baada ya hapo wamecheza michezo sita mfululizo wakishindwa kupata ushindi, walifungwa na Dodoma Jiji bao 1-0, kisha wakachapwa 2-0 na Ruvu Shooting.

Wakafungana 1-1 na Ihefu wakiwa nyumbani, wakaja kufungwa na Young Africans kwa Mkapa kwa bao 1-0. Wakatoka sare na Biashara United nyumbani, kisha wakafungwa na Gwambina 2-0 wakiwa nyumbani pia.

Kwenye msimamo wanashika nafasi ya 14 wakiwa na pointi zao 24 wakiwa wamecheza michezo 22, wameshinda mechi sita, sare katika michezo sita, wakichapwa mabao 10.

Akizungumzia matokeo hayo kocha wa timu hiyo Hitimana Thiery amesema: “Siyo matokeo rafiki kwetu, nafikiri kutopata wachezaji mbadala wakati wa dirisha dogo ilikuwa sababu nyingine inayotugharimu kwa sasa. Tunapambana kuweka mambo sawa.”

SOMA NA HII  RASMI LIGI KUU BARA KUITWA NBC PREMIER LEAGUE