Home Yanga SC PLUIJM ANA JAMBO NA YANGA

PLUIJM ANA JAMBO NA YANGA


MOJA ya makocha ambao wapo kwenye nafasi nzuri ya kupewa nafasi ya kuinoa Yanga msimu ujao ni kocha wa zamani wa timu hiyo raia wa Uholanzi, Hans Van Pluijm.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinasema kuwa Hans ameingia kwenye 10 bora ya makocha ambao wameshapewa kipaumbele cha kuinoa timu hiyo, ambapo jina lake limepitishwa kwenye mchujo wa kwanza. 

Mtoa taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga amesema: “Mchakato wa upatikanaji wa kocha mkuu bado unaendelea, tayari majina manne yamepita kwenye mchujo wa kwanza, ambapo kwenye mchujo huo yupo pia kocha wetu wa zamani Hans Van Pluijm.

“Kilichombeba Hans ni kwa sababu ya mafanikio yake makubwa aliyoyapata akiwa na timu hiyo miaka ya nyuma, lakini pia ikumbukwe kocha huyo alikuwa mwanachama wa timu hii na anaifahamu nje ndani timu yetu.

“Analijua soka la Tanzania na Afrika vizuri kabisa, kwa sababu alishafundisha kwetu, akaenda Singida United, Azam FC na baadae akaondoka zake kwao, hivyo jina lake lipo mezani na atakuwepo hadi kwenye mchujo wa mwisho,”

Alipotafutwa Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro ili kupata undani wa dili hilo alisema: “Kwa sasa naomba mambo yote kuhusu klabu hasa ili la kocha mkuu, watu wasubiri au waisikilize zaidi taarifa itakayotolewa na klabu, siyo vema kuanza kuhisi au kuzungumza vitu ambavyo pengine siyo vya kweli.”

Yanga ipo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mkuu baada ya kuachana na Cedric Kaze na sasa timu hiyo ipo chini ya kocha wa muda Juma Mwambusi.

SOMA NA HII  ALIYEIMALIZA SIMBA KWA MKAPA APANIA KUFUNGA SANA