Home Habari za michezo KIMENUKAAH…CAF WAANZA KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA WASAUZI KUHUSU VAR KUZIMWA KWA MKAPA…

KIMENUKAAH…CAF WAANZA KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA WASAUZI KUHUSU VAR KUZIMWA KWA MKAPA…


Shirikisho la soka Africa (CAF) limeanza uchunguzi kuhusu malalamiko ya kocha wa Orlando Pirates kuhusu mchezo wa Simba dhidi Orlando uliofanyika katika Dimba la Mkapa Dar es Salaam, Jumapili Aprili 17, 2022.

Kocha wa Orlando Mcikazi alilalamika kuwa mfumo wa Video Assistance Referee (VAR) ulizimwa kwa makusudi na haukutumika.

Katika mchezo huo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0, bao pekee la mkwaju wa penati lililofungwa dakika ya 68 na nahodha msaidizi wa Simba, Shomari Kapombe.

Simba watacheza mchezo wa marejeano na Orlando nchini Afrika Kusini, Jumapili ya wiki hii, Aprili 24.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO..SIMBA WATAMBA NA LENGO LILE LILE LA 'KUSAFISHA JALALA'...