Home Habari za michezo UCHAGUZI MKUU SIMBA: WAPIGA KURA WAGOMA….KAMATI YAINGIA ‘CHOBINGO’…

UCHAGUZI MKUU SIMBA: WAPIGA KURA WAGOMA….KAMATI YAINGIA ‘CHOBINGO’…

Mkutano Mkuu Simba

Wapiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Simba wamegomea uamuzi wa kamati ya Uchaguzi wakati wa kuchagua wajumbe.

Kamati hiyo ambayo imeenda kujipanga, ilipofika saa 9.45 mchana ilitoa tamko la kupiga kura kwa mjumbe mmoja kati ya 12 wanaowania nafasi tano, moja ikiwa mwanamke.

Tangazo la kamati limetaka kila mpiga kura kuchagua mjumbe mmoja tu, kisha baadae atakayekuwa na kura nyingi ndiye atakuwa mshindi.

Tangazo hilo liliibua zomea zomea ukumbi mzima wapiga kura wakipaza sauti kuwa hawataki.

Katiba inaruhusu kuchagua wajumbe watano, kwanini tuchague mmoja, hatutaki, ilikuwa ni kauli za wanachama ndani ya ukumbi huo.

Kamati imekwenda chemba kujadiliana upya jambo hilo lililokataliwa na wapiga kura hao

SOMA NA HII  FT: YANGA 2-0 SINGIDA BIG STARS.....KWA MAKALI HAYA YA GAMONDI...SIMBA TAFUTENI SABABU MAPEMA...